Includes unlimited streaming via the free Bandcamp app, plus high-quality download in MP3, FLAC and more.
Purchasable with gift card
$0.50USD or more
lyrics
VERSE 1: DoubleOMsome
Kile unachokipenda siku zote sio rahisi ukipate/
Kama kinyesi hadharani we ndio nzi nenda uifwate/
Wengi wanaochukizwa ni ukweli watatema mate/
Hamu iliyo na ladha ndio huifanikisha shibe siagi unapoipakakwenye mkate/
Vikwazo ndio hujenga msingi/
Nayo imani kwenye penzi ndio itakuondolea vigingi/
Ni bora usingizini wewe uhame/
Usichoke ikimbiza ile ndoto yako ya tangu mtoto/
Safari imejaza msoto kama viunzi chini moto/
Ambatana na nafsi yako kama kulwa na doto/
Harusi isiyo halali ni ukikosa mvuto wa moyo/
Unachopenda huwa ni mwito mwenzio akijaribu huhisi uzito/
Ramani huwa ni moja ila dira ndio kuu hoja/
Weka mtazamo ndio ukuongoze upae juu kwa umakini we rubani/
Na sio kuelekea popote kama moshi wa kiko unavyotanda juu hewani/
Ya dunia huwa mazito haswa ukiyabeba mabegani/
Bora uzingatie ya moyo ikijipa utakwepa uchoyo/
Sahani moja mkishare nae kibogoyo/
Amini ya kwamba ukipotea ndio unajua zako dua ndio kivuli/
Kama ukipenda tendo hazizuiliki hisia kwa miavuli/
Ni bora maoni we uyachuje makufuli ya woga ndio utavunja/
Nawe utaloa mema kwa jinsi Baraka zinavyokuja/
CHORUS: PETIT MAKAMBO
Usikate tamaa maisha ni kupambana bwanaa
Usikate tamaa siku yako itafika bwanaa
Eeeh ni kupambana
Eeeh jitume bwanaa
Eeeh ni kupambana
BRIDGE: PETIT MAKAMBO
Usikate tama maisha
Maana Mungu ndiye anayetoa riziki zetu bwana
Onyesha bidii kwa kila jambo unalolifanya
Waheshimu ndungu rafiki waonyeshe upendo kwanza
VERSE 2: DoubleOMsome
Maisha kitendawili aliye na mwili bila akili/
akakope za wakili kuzaliwa sio mara mbili/
bila kejeli utaishi kwa maadili usibadili mola alivyokusajili/
kwa matamu na mkali ndivyo iliyo hali/
Uwe karibu au mbali jua jalali halali/
kwenye mashaka kamwe wee muulize swali/
kama mfuasi wa jumapili mwaminie kwa hali na mali/
mchizi utapata zali jipe moyo sista na chali/
Msichoke fwata nyuki mwisho mtapata asali/
Usishiriki ushirikina kaza msuli kwa kusali ju Mola anakujali/
Usiruhusu kibali cha majuto kichwani kwani hutobadili mienendo kama awali/
Sukuma wiki na ugali iko siku ya wali hutojulishwa kama ajali/
Tembea kama jangili wakuvishe bangili iko siku ya ndege utazuru hata Kigali/
Usilaumu getto iko siku ya Nyali utapewa saluti kama major Hussein Ali/
Msoto una asili usiojali bora tuwe na roho kama jabali/
Kweli utafika mbali ukishamega la halali/
mwenzio mpoze hali usiwe mlafi na bahili/
ukumbuke ulikotoka hata ikiwa kitalii/
Dua njema na fanaka utapoke za Jalali/
Kijeshi jeshi usife moyo pigana na hali usijepotezwa kwenye hili jedwali/..
CHORUS: PETIT MAKAMBO
Usikate tamaa maisha ni kupambana bwanaa
Usikate tamaa siku yako itafika bwanaa
Eeeh ni kupambana
Eeeh jitume bwanaa
Eeeh ni kupambana
credits
released August 23, 2017
ft: Petit Makambo
producer: Crash
Crack Sound Studio